Jeshi la Polisi Arusha limewaua majambazi watatu waliokuwa wakihusika na matukio ya wizi, pia liliwakuta wakiwa na milipuko ya bovu, bunduki, mavazi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na ujumbe maalum kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Dar es salaam, Suleiman Kova.
Ujumbe uliandikwa ‘Nasaha kwa Kova, Mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe‘
Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas amesema ‘Jeshi la Polisi Arusha lilipata taarifa kuwa kuna mtu wanamuhisi ni mharifu, tukaweka mtego na kumkamata mtu mmoja, tulipofanya msako katika chumba chake na kukuta milipuko kadhaa‘
‘Marushiano ya risasi yakaanza kufanyika na hatimaye Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi, jitihada za kuwapeleka hospitali zilishindwa kwasababu watu hao wote walifariki wakati wakipelekwa hospitali ‘

0 Comments
Post a Comment